
Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Tundu Lissu
Akihutubia umati uliojitokeza kusikiliza sera zake leo, Lissu amewashukuru wananchi hao kwa maombi, misaada pamoja na sala zao kwa kipindi chote cha miaka mitatu alichokuwa akikipitia.
"Nawashukuruni sana kwa maombi yenu, kwa misaada yenu ya kila namna,kwa sala zenu katika kipindi hiki cha miaka tatu nilichokipitia dhidi ya nyie, ndugu zangu wa Babati zimebaki siku kumi mtapiga kura katika mazingira hayahaya" alisema Lissu
Aidha Lissu, ameendelea kuwahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo tarehe 28 mwezi huu huku akiainisha baadhi matukio ambayo hutokea katika siku ya uchaguzi ikiwemo ya mawakala kutokuruhisiwa kuingia vituoni ambapo amesema kwa mwaka huu kwa mujibu wa kanuni za Tume ya Taifa ya Uchaguzi barua ya utambulisho wa mawakala zitapelekwa na Mkurungenzi wa uchaguzi katika vituo.
Leo Lissu anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mkoani Manyara na Arusha ambapao ataendelea kunadi sera zake.