Wednesday , 21st Oct , 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu kuhakikisha leo Oktoba 21, 2020, vinakabidhi orodha ya mawakala wa vyama vyao kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume wa Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage

Hilo limewekwa wazi na Mwenyekiti wa Tume wa Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage baada ya kumaliza siku ya kwanza ya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuhabarisha masuala ya uchaguzi.

''Vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vinatakiwa kuhakikisha Jumatano Oktoba 21, 2020, vinakabidhi orodha ya mawakala wa vyama vyao kwa wasimamizi wa uchaguzi kote nchini'', alisema Kaijage.

Aidha katika hatua nyingine Kaijage aliweka wazi kuwa majumuisho ya kura za urais katika uchaguzi wa Oktoba 28, 2020 yatafanyika Dar es salaam na sio Dodoma ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Tume kwenye jengo la Uchaguzi House.

Mafunzo kwa waandishi wa habari yanaendelea leo Oktoba 21, 2020 jijini Dar es salaam.