Thursday , 22nd Oct , 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amewaagiza wakandarasi waliopewa kazi ya ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa 4 kuhakikisha kwamba ujenzi huo unamalizika kwa wakati kama mkataba unavyowaelekeza na serikali itafuatilia kwa karibu ili kusitokee suala la kuongeza muda.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James.

Katibu Mkuu James ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa miradi ya ukarabati na ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa ya Tabora, Sumbawanga, Shinyanga na Kigoma miradi ambayo hadi kukamilika kwake zaidi ya shilingi bilioni 136 zitakuwa zimetumika.

Awali akitoa maelezo ya namna miradi hiyo itakavyotekelezwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale amesema miradi hiyo inakwenda kukuza biashara kwa kuwa ndege kubwa sasa zitaweza kutua katika viwanja hivyo.