
Lionel Messi (kushoto) na Cristiano Ronaldo (kulia)
''Kuna mijadala mingi juu ya ubora wa wachezaji hao, wengi wanabishana nani ni zaidi ya mwenzake kwa maoni yangu siwezi kusema nani ni zaidi kati ya wawili hao, ila ninachoweza kusema ni vigumu kwa wachezaji wengine wa sasa kufikia viwango vyao'', alisema Maradona.
Maradona nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina na vilabu kama, Barcelona na Napoli alicheza kwa kiwango cha juu wakati wake huku akishindanishwa na gwiji mwenzake kutoka Brazil Edson Arantez do Nascrimento maarufu kama Pele
Dunia haikuwahi kupata jibu la moja kwa moja nani alikuwa zaidi, kati ya Pele na Maradona, hivyo alivyoulizwa yeye alishindwa kusema nani ni zaidi ya mwenzake zaidi ya kusema hakuna wachezaji wengine watakao wafikia hawa wawili
Ikumbukwe kuwa Maradona na Messi wote ni Waargentina, na walipata kufanya kazi pamoja kwenye kombe la dunia la mwaka 2010 kule Africa kusini moja akiwa kocha na mwingine akiwa mchezaji lakini alishindwa kusema yupi ni bora.