
Cindy ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuachana na Mario ambaye walidumu naye katika mahusiano kwa muda mrefu, kwa sasa amejituliza kwa Ken wakiwa katika hatua za awali kabisa za mahusiano wakiwa na changamoto kutoka kwa Phina ambaye ameapa kumpigania Ken kumrudisha katika mikono yake.
Ken ambaye naye tayari amekwishaonekana kukolea kwa Cindy sasa, amesema kuwa ataendelea kumhudumia mtoto wake ambaye amempata akiwa na Phina, ila hana mpango wa kurudiana na mwanadada huyu hata kidogo.