Saturday , 7th Nov , 2020

Kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 kinatarajiwa kuanza Novemba 10 mwaka huu kama ilivyotamkwa kwenye tangazo la Rais ambapo katika mkutano huo shughuli sita zitafanyika.

picha ya Bunge

Akizungumza na wanahabari katika ofisi ya Bunge, Katibu wa Bunge STEPHEN KAIGAIGAI amesema shughuli ambazo zitafanyika ni kusomwa kwa tangazo la kuitisha Bunge, Uchaguzi wa Spika, Kiapo cha uaminifu kwa wabunge wote, kuthibitisha uteuzi wa waziri mkuu, uchaguzi wa naibu Spika na ufunguzi rasmi wa bunge.

''Tunawasisitizia wabunge wateule wote wanapokuja wafike wakiwa na hati ya kuteuliwa kuwa mbunge,kitambulisho cha Taifa na kadi ya benki yenye akaunti namba ya mbunge''amesema Stephen Kaigaigai