Tuesday , 10th Nov , 2020

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amemteua chipukizi Jude Bellingham toka Borussia Dortmund kujiunga na kikosi chake

Chipukizi Jude Bellingham anayekipiga Borusia Dortmund

 

Bellingham anachukua nafasi ya mlinzi James Ward Prowse anayekipiga katika klabu ya Southampton mwenye kiwango bora kwa sasa, amelazimika kujiondoa katika kikosi hicho, kwa sababu ya majeraha

Kuteuliwa kwa Bellingham kunamfanya ashike rekodi ya tatu kwa mchezaji chipukizi wa England kuchezea kikosi hicho hasa kama atapata nafasi ya kucheza katika mechi ijayo dhidi ya Ireland alhamisi hii ya tarehe 12 Novemba 2020, atakua anatimiza umri wa miaka 17 na siku 136,

Rekodi ya kwanza inashikiliwa na Theo Walcott aliyoiweka mwaka 2006 katika mchezo dhidi ya Hungary, ambapo alicheza akiwa na umri wa miaka 17 na siku 75 inafuatiwa na Wayne Rooney aliyeweka rekodi ya kucheza dhidi ya Uturuki mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 17 na siku 111