Wednesday , 11th Nov , 2020

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa Rais Magufuli atalihutubia Bunge na Taifa siku ya Ijumaa ya Novemba 13, 2020, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli za Bunge la 12.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Novemba 11, 2020, wakati akifungua shughuli za Bunge la 12 kikao cha 2, jijini Dodoma, ambapo shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuapishwa kwa baadhi ya wabunge na kwa wale wenye udhuru zoezi la kuapa litafanyika siku za mbeleni.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano anahutubia Bunge kwa maana ya kuweka dira ya serikali yake kwa miaka mitano inayokuja, kwahiyo naomba siku ya Ijumaa, asubuhi tutawaomba waheshimiwa wabunge wote tuwe ndani ya ukumbi huu", amesema Spika Ndugai.

Taarifa kamili inafuata.