
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na msanii Chege Chigunda
Moja ya surprise hizo ni Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwapa kofia baadhi ya wasanii na kucheza muziki pamoja, Chege Chigunda ni mmoja wa wasanii waliopata bahati ya kucheza 'style' ya mapanga shaa na Rais huyo kwenye jukwaa moja.
Akizungumza tukio hilo kupitia kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio Chege amesema kuwa "Mheshimiwa alihama jukwaa la waheshimiwa akanifuata kumaliza show na mimi, wakati Rais ananifuata jukwaani nikazuiliwa ila yeye akasema niachiwe nikacheza naye"
Aidha ameendelea kusema "Nimegundua watu wa siasa wapo mbali na muziki ila wanaupenda, hakuna lawama mpya kwenye siasa lawama zote zimetumika, mimi sina utaalam wa kugombea nafasi za siasa".