Thursday , 12th Nov , 2020

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kupendekezwa kwake kwa mara nyingine tena kuwa Waziri mkuu wa Tanzania na Rais John Pombe Magufuli si jambo dogo huku akimshukuru kwa kumpendekeza kwa mara nyingine tena.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

Akizungumza mara baada ya kupendekezwa na kuidhinishwa na wabunge wa bunge la 12 kupitia upigaji kura uliofanyika leo bungeni, Dodoma, Majaliwa amewashukuru wabunge wote kwa kumpigia kura nakuwahakikishia kuwa watafanya kazi pamoja.

“Jambo hili si dogo, namshukuru sana kwa imani yake kubwa aliyonayo juu yangu nakuendelea kuniamini kwamba naweza kufanya niliyofanya katika kipindi cha miaka mitano na zaidi katika kipindi kingine kijacho" amesema Majaliwa

Majaliwa ameongeza pia, "Niendelee kumhakikishia kwamba matamanio yake yaliyompelekea kutoa jina hilo kulileta mbele ya bunge hili tukufu ambayo anaamini na wabunge wenzangu kwa namna ambavyo mmepiga kura nyingine ni namna tosha mheshimiwa rais ameleta jina ambalo mnaamini nitamsaidia kazi, na mini  niwahakikishie nitafanya hivyo"

Leo Rais Maguful,i amempendekeza mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa muhula mwingine tena huku wabunge wakimpigia kura 350 kati ya 354 na kuonyesha kuridhishwa na pendekezo hilo la Rais lililowasilishwa na mpambe wake bungeni Dodoma.