
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo hii leo, Novemba 12, 2020, Bungeni Dodoma, mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa kumchagua Naibu Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson, aliyepata kura za ndiyo 350 na kura za hapana 4.
"Jamani matokeo nimekwishayapata kutoka kwa katibu, kwamba hakuna kura zilizoharibika, safari hii hili Bunge ni la wasomi watupu hakuna kura inayoharibika, na wabunge waliopiga kura ni 354", amesema Spika Ndugai.
Dkt. Tulia Ackson, anashika wadhifa wa Unaibu Spika kwa awamu ya pili sasa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.