Thursday , 12th Nov , 2020

Nahodha wa Arsenal na timu ya Taifa ya Gabon Pierre Emerick Aubameyang amekodi ndege binafsi ya kifahari, kumpeleka nyumbani kwao Gabon kwa ajili ya mchezo dhidi ya Gambia wa kufuzu kombe la mataifa ya Africa.

Pierre Aubameyang akishangilia goli alilofunga dhidi ya Manchester United

Aubameyang kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya kikosi cha Arsenal, akitajwa kupokea zaidi ya fedha za Kitanzania  bilioni moja kwa juma, na kuwa miongoni mwa wachezaji wa Kiafrika wanaolipwa vizuri Ulaya.

AFCON imekuwa na msisimko mkubwa tangu kuanza kwake 1957, kwa kuwa inakutanisha wachezaji bora wa Kiafrika wanaocheza ndani ya bara na nje ya bara, na limekuwa jukwaa pekee la kuoneshana umwamba kwa mataifa ya Afrika.

Gabon ipo kundi D lenye timu za Gambia, DR Congo pamoja na Angola, ikiwa na alama 4 sawa kabisa na Gambia yenye alama 4 pia, huku wakitofautiana wastani wa magoli, kwa maana hiyo hii mechi ina umuhimu mkubwa sana ndani ya kundi hilo.