
Wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Daz Nundaz kushoto, kulia ni Producer P Funk Majani
P Funk Majani ametumia ukurasa wake wa mitandao wa kijamii kama Twitter na Instagram, kutoa ujumbe huo baada ya wimbo wa kundi hilo uitwao kamanda uliotoka mwaka 2001 kufikisha wasikilizaji laki 1 kwenye mtandao wa Boom Play ambao una 'deal' kwa kuuza na kusikiliza nyimbo.
"Ahsanteni kwa support, Ferooz na Daz Baba acheni utoto pigeni kazi ya pamoja mrudishe bendera ya Daznundaz"
Kundi hilo lilikuwa linajumla ya wasanii watano ambao ni Ferooz, Daz Baba, Critic, La Rumba, and Sajo na walifanikiwa kutoa nyimbo ambazo zilifanya vizuri kipindi cha nyuma kama elimu dunia, kamanda, barua, boss na kamanda.