
Meson Mount wa Chelsea
Kueleke kwenye mchezo huo Kocha wa Chelsea Frank Lampard huenda akawarejesha kikosini washambuliaji wake Hakim Ziyech na Callum Hodson Odoi baada ya nyota hao kupona majeraha yao na kufanya mazoezi ya pamoja na timu tokea ijumaa ya juma lililopita.
Mchezo huo unatazamiwa kuwa wenye upinzani mkali pale ambapo Chelsea anahaha kusaka ushindi kwa hamu kubwa mara baada ya kupoteza michezo yake miwili mfululizo kwenye EPL na wakati huo huo Westham wakitaka kuendeleza wimbi la ushindi kwa kutokupoteza mchezo.
Kwa Upande wa Westham, Kocha wake David Moyes yupo njia panda baada ya kukosa jibu la moja kwa moja kama mshambuliaji wake Michael Antonio atakuwa fiti kuwavaa Chelsea baada ya nyota wake huyo kuwa nje ya uwanja tokea mapema mwezi Novemba.
Wachezaji wa West Ham
Chelsea ambayo ipo nafasi ya 8 hivi sasa baada ya kujizolea alama 22 baada ya michezo 13, imepoteza mchezo 1 pekee kati ya 14 ya mwisho waliyocheza kwenye dimba lake la nyumbani dhidi ya Westham, Mchezo mmoja waliopoteza wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0 msimu uliopita
Kama Chelsea atapoteza mchezo wa hii leo ataweka rekodi ya kupoteza michezo mitatau mfululizo ya EPL kwa mara ya kwanza tokea Novemba mwaka 2015 na kupoteza mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Westham kwa mara ya kwanza tokea Februari 1996.
Westham ipo nafasi ya 10 baada ya michezo 13 nakufikisha alama 21, utofauti wa alama1 na wapinzani wao wa hii leo Chelsea.
Mchezo mwingine wa EPL utakaopigwa hii leo ni ule utakaowakutanisha Burnley waliopo nafasi ya 18 wakiwa na alama 10 uso kwa uso na Wolves waliopo nafasi ya 10 wakiwa na alama 21 mchezo utakaochezwa saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.