
Picha ya Shilole na mpenzi wake Rommy 3D
Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Shilole amesema hakutegemea na hakuamini kama atavalishwa pete hiyo ya Almasi na mwanaume ambaye amempambania kwa nguvu zote.
"Sikutegemea na sikuamini kabisa, nilikuwa na taharuki na nilistuka kwa kweli kwa sababu haikuwa tegemeo maana mimi nilikuwa na jambo langu mwenyewe la kujizawadia gari hata mwanaume mwenyewe hakuwa na dalili ya kunivalisha pete pia sikuwa nimefikiria hivyo vitu, ila sasa hivi hapa nina pete yangu ya Almasi kwenye kidole changu" amesema Shilole
Aidha Shilole amesema yupo tayari kwa ndoa ya pili endapo na ikimpendeza Mungu basi wataoana kwa sababu kuolewa kwa mwanamke ni sunnah.