
1. Mwana Fa na Babu Tale kuingia Bungeni, Prof Jay na Joseph Mbilinyi kutoka
Mwaka 2020 kulikuwa na tukio kubwa la kitaifa ambalo ni Uchaguzi Mkuu na kupiga kura ili kuchagua viongozi watakaoongoza kwa miaka mitano ijayo kwenye ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais, ambapo tumeona wasanii wengi na watu maarufu walijitokeza kutia nia ya kugombea Ubunge.
Bahati imekuwa nzuri kwa msanii wa HipHop Mwana Fa, baada ya wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi 'CCM' na Muheza, Tanga kumpa ruhusa ya kuingia Bungeni kwa mara ya kwanza ili kuwawakilisha.
Mwingine alikuwa ni Hamisi Taletale 'Babu Tale' ambaye amepita bila kupingwa kuongoza watu wa Kusini Mashariki mwa Mkoa wa Morogoro kupitia CCM.
Aidha Wanasiasa na wasanii wakongwe wa HipHop Bongo Joseph Mbilinyi 'Mr II Sugu' na Joseph Haule 'Prof Jay' wameshindwa kurudi kutetea viti vyao vya Ubunge baada ya kura zao kutotosha.
Wote hao walikuwa wanatokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo Joseph Mbilinyi alikuwa anaongoza Jimbo la Mbeya Mjini kuanzisa 2010 - 2020, huku Prof Jay aliiongoza Jimbo la Mikumi kuanzia 2015-2020.
Itaendelea.....