Friday , 1st Jan , 2021

Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba imewataka wanachama wa klabu wenye mapingamizi dhidi ya mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu wawasilishe mapingamizi kwenye ofisi za klabu zilizopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam kabla ya tarehe 2 Januari mwaka huu.

Picha ya jengo la Simba lililopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Kamati imetoa taarifa hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kutoa orodha ya majina manne ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti kwenye Uchaguzi unaotaraji kufanyika tarehe 7 mwezi huu. Majina ya wagombea hao yameorodheshwa kwenye taarifa iliyotolewa na Simba hapo chini.