Monday , 18th Jan , 2021

Mshauri wa masuala ya mahusiano na ndoa Melisa Kasembe, amesema kuwa ndoa ni taasisi iliyoanzishwa na Mungu, hivyo mwanamke yoyote akiingiza masuala ya kiuanaharakati kwenye ndoa yake basi lazima itamshinda.

Melisa Kasembe, Mshauri wa masuala ya mahusiano

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ cha East Africa Television, kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kuongeza kuwa suala la ndoa linafuata misingi ya dini na siyo misingi ya kiuanaharakati.

"Ndoa ni taasisi iliyoanzishwa na Mungu, haikuanzishwa na serikali, haikuanzishwa na chama cha siasa, kwahiyo kama ilianziswa na Mungu ina misingi yake, mwanamke aliitwa msaidizi haibadiliki ndiyo maana ukijiweka kwenye mambo ya uanaharakati ndoa itakushinda kwa sababu haina misingi ya kiuanaharakati ina misingi ya kidini, ndiyo maana hata serikali inafuata misingi ya kidini linapokuja suala la ndoa, serikali haina misngi yake ya ndoa", amesema Melisa

Tazama video hapa