Friday , 22nd Jan , 2021

Klabu ya Manchester City imepata pigo kufuatia taarifa za kiungo wake Kevin de Bruyne kuripotiwa kuwa atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne hadi sita kutokana na maumivu ya misuli ya paja.

Kevin de Bruyne akiugulia maumivu .

Raia huyo wa Ubelgiji aliumia wakati wa mchezo kati ya Manchester City dhidi ya Aston Villa ambao ulimalizika kwa The Citizen kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

Kuumia kwa nyota huyo kunamaanisha atakosekana katika michezo mitatu ijayo ambayo Manchester City itakabiliana na Liverpool, Tottenham Hotspurs na Arsenal katika ligi kuu.

Nyota huyo ndiye kinara wa pasi za mwisho za mabao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo hadi anaumia alishatengeneza nafasi 10.

Manchester City kwa sasa inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL kwa alama zao 38 nyuma ya vinara Manchester United wenye alama 40.