Monday , 25th Jan , 2021

Rais Dkt. John Magufuli, amemuomba Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde, kukirudisha kiwanja ambacho kilitengwa kwa ajili ya Tanzania kujenga Ubalozi wake chini humo na kunyang'anywa kwa kushindwa kukiendeleza, baada ya pesa zilizotumwa kuliwa na aliyekuwa Balozi wa wakati huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 25, 2021, mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo ya faragha na Rais huyo yaliyohusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kuahidi kwamba kama nchi ya Ethiopia itakirudisha kiwanja hicho basi serikali itahakikisha inakiendeleza.

"Nimemueleza pia ombi letu dogo kwenye uwanja wetu kule Ethiopia ambao tulichelewa kuujenga kwa sababu ni ukweli, zile hela tulizozipeleka kule kujenga zililiwa na Balozi wetu huko, siyo huyu anayekaimu Ubalozi, ni aliyekuwepo na tukamrudisha nyumbani kwahiyo tukawa tumechelewa kuenga", amesema Rais Magufuli.

"Tukashindwa kuzingatia masharti ya sheria za kule kwamba, kiwana ukipewa na usikiendeleze unanyang'anywa, tumemuomba Mh. Rais aturudishie na tumeahidi tutakiendeleza kwa kukijenga  na pale Dodoma tumewapa hekari tano na wao waziendeleze kwa kujenga ubalozi wao", ameongeza Rais Magufuli.