
Msanii wa HipHop Stamina
Akizungumzia hilo kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, Stamina amesema alishangazwa na kitendo hicho kwani hakutegemea kama mpenzi wake huyo atafanya jambo hilo kwa zaidi ya mikoa 15.
"Ukiachana na mama mzazi siku ya wanawake duniani naipeleka kwa Mama Lionel, kipindi nakutana naye sikutegemea kama ni mpambanaji alinishangaza kwani nilikuwa na ziara zangu za chaka kwa chaka za mikoani akasema twende wote, yeye alikuwa anakaa getini kuchua pesa wakati nafanya show kwenye jukwaa na alikuwa anawakazia kinoma noma" ameeleza Stamina
#MwanamkeKinara