
Raisi Mteule wa CAF Patrice Motsepe
Motsepe raia wa Africa kusini, amechanguliwa na wajumbe waliokuwa na sifa ya kupiga kura mbele ya ushuhuda wa Rais wa shirikisho la soka duniani 'FIFA' Giann Infantino, uchaguzi unaotajwa kuwa huru na wa haki ukizingatia alikuwa mgombea pekee.
Rais huyo mpya wa CAF atalazimika kutimiza ahadi zake alizozitoa kama kipaumbele chake wakati wa kampeni, miongoni mwa ahadi hizo ni
1 Kuwekeza katika maendeleo na ukuaji wa soka la Africa kwa wadau na washirika mbalimbali.
2 Kuongeza ubora na ufanisi ikiwemo uweledi wa hali ya juu katika mashindano ya mbalimbali ya CAF.
3 Kufanya kazi kwa uwazi hasa katika mapato na matumizi ya CAF
4 Kuweka miundombinu mbalimbali katika kiwango cha kimataifa, ikiwemo kujenga maeneo 200 ya kuchezea 'pitches'
5. Kuwekeza katika soka la vijana ambalo lina dira ya mpira wa Africa kwa wakati ujao
6 Kupandisha kiwango cha soka la wanawake katika maeneo yote muhimu utawala kiufundi, uamuzi.
7. Kufanya kazi kwa ukaribu na FIFA