
Erling Haaland mshambuliaji bora kijana wa Dortimund anayetarajiwa kung'aa katika hatua zijazo za ligi ya mabingwa
Bayern anafuzu kwa jumla ya ushindi wa 6-2 baada ya kupata ushindi wa 4-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza na 2-1 katika mechi ya mkondo wa pili, huku Chelsea wakifuzu kwa jumla ya bao 3-0 baada ya ushindi wa mkondo wa kwanza 1-0 na pia mechi ya mkondo wa pili 2-0 na kumaliza utawala wa timu hiyo kucheza misimu 7 mfululizo hatua hiyo ya robo finali.
Timu zilizofuzu katika hatua hii ya robo ni Borussia Dortmund, Bayern Munich toka Ujerumani, Manchester City, Liverpool, Chelsea toka Uingereza, PSG kutoka Ufaransa, FC Porto ya Ureno na Real Madrid ya Uhispania.
Droo inatarajiwa kupangwa ijumaa hii tarehe 19/03/2021 makao makuu ya shirikisho la soka la Ulaya 'UEFA' yalipo Nyon Uswis, ambapo robo fainali inatarajiwa kufanyika tarehe 6/7 mwezi wa 4 kwa mechi za mkondo wa kwanza na zile za mkondo wa pili zitachezwa tarehe 13/14 mwezi huo huo wa 4.
Nusu fainali zimepangwa kuchezwa tarehe 27/28 mwezi wa 4 kwa mechi za mkondo wa kwanza, huku zile za mkondo wa pili mechi zikitarajiwa kuchezwa 4/5 mwezi wa 5 na fainali imepangwa kuchezwa tarehe 29 mwezi wa 5 katika uwanja wa Ataturk Olympic Istanbul Uturuki.