Friday , 26th Mar , 2021

Leo Machi 26, 2021, ndiyo inahitimishwa safari ya hapa duniani ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, ambapo atapumzishwa kwenye makaburi ya familia yaliyopo nyumbani kwake Chato.

Mwili wa Hayti Dkt. John Magufuli, ukipigiwa saluti na wanajeshi

Kabla ya mazishi ambayo yatafanyika saa 10:00 jioni ambayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, baadhi ya watu watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho mara baada ya misa takatifu ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli inayofanyika katika uwanja wa Magufuli uliopo Rubambagwe Chato.

Ambapo baadaye Rais Samia ataongoza familia na viongozi kuelekea eneo la mazishi ambapo ibada ya mazishi itaongozwa na Askofu Severine Niwemugizi.

Hayati Dkt. John Magufuli, alifariki dunia Machi 17, 2021, jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Mzena kutokana na maradhi ya moyo