
Mhe. Humphrey Polepole
Polepole ameuliza swali hilo kwenye kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Machi 31, 2021.
''Uzalishaji wetu wa Soya Bean ni mdogo sana na tumeshaingia mkataba wa kupeleka tani laki 4 nchini China lakini uzalishaji wetu kwa mwaka unaonekana kuwa tani elfu 14, serikali imejipanga vipi kutumia soko hili kubwa litakalo leta tija kwa wakulima Tanzania?” aliuliza Mhe. Polepole.
Swali hilo la Polepole limejibiwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ambaye ameeleza kuwa tayari serikali imeshaanza kuweka utaratibu wa kupata mbegu bora ili kuwasaidia wakulima kufikia lengo la uzalishaji wa Soya Bean ili kulinda soko hilo.
''Kwa hatau ya awali tuliyochukua kulinda soko hili, tumeamua kuondoa mifumo ya ukiritimba kwa kuwasajili wafanyabiashara kwa ajili ya 'export' na kwa kuwa soko lipo na wafanyabiashara wapo, wakulima wenyewe wataongeza uzalishaji watakapopata mbegu za uhakika ambazo wizara tunaanza kuzifanyia kazi,'' amesema Mh. Bashe.