
Pique amerejea mazoezini baada ya kuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja akiuguza majeraha ya mguu aliyoyapata wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Spanish Copa del rey mwezi mmoja uliopita.
Taarifa ya Pique kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake imekuwa taarifa nzuri kwa wanacatalunya kwani April 10, 2021 wanamchezo na mahasimu wao, Real Madrid kwenye ligi kuu nchini Hispania maarufu 'La Liga'.
Barcelona imeeleza kuwa, utimamu na utayari wa Gerrard Pique utajulikana siku ya Jumatatu ambapo Barcelona watakuwa na mchezo dhidi ya Real Valladolid kama nyota huyo atacheza ama laa licha ya kocha wa klabu hiyo Reonald Koeman kusema hawatomharakisha mkongwe huyo kurejea dimbani.