
Kushoto ni msanii Lord Eyes, kulia ni mtangazaji Billsepenga
Billsepenga ametoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagrama ambapo ameeleza kuwa.
"Alfajiri ya leo nimeshambuliwa na kudhalilishwa na maeneo ya Masaki na msanii Lord Eyes, nimefungua kesi Oysterbay na nikipatwa na tatizo lolote naomba yeye awe mtuhumiwa wa kwanza kwa kibaya kitachonitokea ( Joh Makini, Nikki wa Pili Lord Eyes na Gnako Warawara ) ahsante" ameandika Billsepenga
EATV & EA Radio Digital, imejaribu kumtafuta Billsepenga atoelee maelezo kuhusu chanzo cha tatizo hilo lakini kwa bahati mbaya hakuweza kushika simu yake.