Saturday , 24th Apr , 2021

Kocha mkongwe wa mpira wa kikapu Nchini Tanzania Bahati Mgunda amesema Kinacho wakwamisha vijana wengi kukosa nafasi za kwenda kucheza mpira wa kikapu nje ya Africa ni kufeli masomo yao na Vimo vyao vifupi.

Atiki Ally Atiki Mtanzania aliyesajiliwa na London Basketball Academy nchini England.

"Vijana wengi wanaocheza mpira wa kikapu Tanzania hawafanyi vizuri kwenye masomo yao na pia wengi wao sio warefu zaidi ya futi 6 na hayo ndio mambo makubwa yanayo wakwamisha kwenda kucheza katika ligi za kimataifa ''Proffessional Basketball" - Kocha Bahati Mgunda.

Mgunda ameyasema hayo wakati akiongea na EATV kuhusu usajili wa mchezaji kinda wa mpira wa Kikapu wa Tanzania Atiki Ally Atiki aliye sajiliwa na London Basketball Academy nchini England.

Atiki Ally Atiki ambaye ni zao la kocha Mgunda tangu mwaka 2014 alimpomuona jijini Mwanza katika mashindano ya vijana ya kikapu  kisha akamleta Jijini  Dar es salaam.

Atiki Ally ni mmoja kati ya Vijana waliopata kucheza na kuonekana kupitia michuano ya kukuza vipaji ya Sprite Basketball Kings msimu wa mwaka 2018 yanayo endeshwa na East Africa TV pamoja na East Africa Radio.