
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi
Dkt. Mwinyi alitangaza uamuzi huo jana Aprili 25, 2021, Ikulu jijini Zanzibar wakati wa hafla ya kuwaapisha Makamanda wapya aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu wa vikosi maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema amefikia uamuzi huo baada ya kubainika kuwa, katika ya mwezi Januari na Machi mwaka huu bodi hiyo imefanya vikao zaidi ya sita na kutumia shilingi milioni 99.7.
“Najiuliza kulikuwa na dharura gani ya kufanya vikao sita ndani ya miezi mitatu, kwa kawaida bodi zinatakiwa kufanya vikao vinne kwa mwaka na ikitokea kuna dharura ndio wanaweza kukutana zaidi ya hapo lakini kuwe na dharura,” amesema Rais Dkt. Mwinyi.
Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa hatosita kuvunja bodi ambazo zimekuwa zikifanya ubadhirifu wa fedha za Serikali.
Zaidi tazama video hapo chini