Sunday , 25th Apr , 2021

Serikali ya Mkoani Lindi imethibitisha kuwakamata watu 7 raia wa Irani wakiwa na tani moja ya dawa za kulevya aina ya Heroin katika eneo la bahari ya Hindi wilayani Kilwa mkoa wa Lindi.

Tani 1 za Heroin Zilizokamatwa Kilwa Mkoani Lindi Siku ya Jana April 24,2021

 

Akizungumza kwa njia ya simu na EATV mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi amesema ni kweli Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na kikosi cha wana maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kimewakamata watu hao siku ya jana.

Ameongeza kuwa raia hao wamewekwa sehemu salama ya ulinzi pamoja na kiasi hicho cha dawa za kulevya kimehifadhiwa vizuri kusubiri taratibu zingine za kisheria.