
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kagera Maketi Msangi
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kagera Maketi Msangi amethibitisha kulifahamu tukio hilo na kudai kuwa hadi sasa wanamsaka mtuhumiwa ambaye alitoroka baada ya tukio.
Akizungumzia tatizo hilo bibi wa mtoto huyo Joines Habibu amesema kuwa siku ya tukio Februari 19 mwaka huu, aliondoka kwenda kanisani na kumuacha mjukuu wake nyumbani kwa mtuhumiwa na kwamba aliporudi wakati akimwogesha mtoto huyo saa nne usiku alianza kupiga kelele akidai anaumia, na kwamba alipofuatilia aliona hali isiyo ya kawaida katika sehemu zake za siri.
Bibi huyo ameongeza kuwa mjukuu wake aliendelea kulia na kuomba apelekwe hospitali, na kwamba alipomhoji maumivu hayo yametokana na nini alimweleza kwamba babu yake ambaye ni baba mdogo wa mama mzazi wa mtoto huyo, alimlaza na kumwingizia kimti kigumu katika sehemu zake za siri.
Bibi huyo aliamua kwenda kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho na kupewa barua ya kwenda polisi kutoa taarifa, lakini hadi sasa mtuhumiwa hajakamatwa.
Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Dk. Mseleta Nyakiroto amesema walimpokea mtoto huyo Februari 20 mwaka huu na kumpatia matibabu ya tatizo alilokuwa nalo ambalo hakulitaja, na kisha kumruhusu.