Monday , 26th Apr , 2021

Klabu ya Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja mlinzi wake wa kati, Erick Bailly jioni ya leo Aprili 26, 2021 kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka mwishoni mwa msimu wa mwaka 2024.

Mlinzi wa kati wa Manchester United, Erick Bailly akisaini mkataba mpya jioni ya leo.

Bailly aliyetua Manchester United mwaka 2016, kandarasi yake ya awali ilikuwa imalizike mwishoni mwa mwaka 2021-2022 lakini kocha wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer amesema amevutiwa na uwezo mkubwa wa nyota huyo na kuamua kumbakisha klabuni hapo.

Baada ya kusaini kandarasi hiyo, Bailly amesema, “Huu ni uamuzi ambao sikuufikira mara mbili, ninapenda kuichezea Manchester United na naipenda hii klabu”.

“Mimi na familia yangu tuna furaha, kila kitu kipo vizuri. Kwasasa vipindi vya kuwa na majeraha kimepita na nina utimamu mkubwa wa mwili na najisikia vizuri. Mkataba mpya ni sawa na changamoto mpya na nipo tayari kwa hilo”.

Bailly amekiri kuendelea kuwa klabuni hapo kw amuda mrefu zaidi kwani kuwa hapo kwa msimu wake wa tano ni kuishi kwenye ndoto zake.

Kuzungumzia nafasi ya klabu yake kubeba mataji, Bailly amesema, “Kwa sasa tupo kwenye nafasi nzuri. Tupo kwenye michuano ya Europa Ligi na tunashika nafasi ya pili kwenye EPL kitu ambacho ni kizuri na tunaimani tutashinda kombe la Europa kwani ni muhimu sana kwa timu na mashabiki”.

Nae kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer hakusita kumwagia sifa beki huyo kitasa na kuweka wazi kwanini aliamua kumsalisha kikosini.

“Erick ameimarika sana kwenye nafasi yake tokea niwe meneja na ataendelea kuwa na nafasi kwenye kikosini. Ana uwezo mkubwa sana wa kucheza kwa kasi, kupora mipira akiwa amelala chini 'Tackle' na amechangamka sana bila shaka ni vitu ambavyo unahitajika mlinzi awe navyo”.