
Walinzi wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu (kushoto) akiwa na Dickson Job (kulia) mazoezini.
Bumbuli ameyasema “Kambi yetu inaendelea vizuri, wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea, Dickson Job pamoja na Abdallah Shaibu Ninja walikuwa na maumivu lakini pia madaktari wanaendelea kuangalia afya ya Carlinhos kwa karibu zaidi na baada ya muda tutatoa taarifa”.
“Lakini so far tunaendelea vizuri na maandalizi na mchezo wetu wa derby ni mchezo mkubwa ambao unasimamisha Dunia kutazama Dunia kuitazama Tanzania inafanya nini kwenye mpira wa miguu”
“Kwahiyo sisi tunajiandaa kuelekea kwenye mchezo huo kuhakikisha kwamba siku ya mchezo Dunia inaona kwamba kweli Yanga ni moja ya timu kubwa barani Afrika, Yanga ni moja ya timu kubwa Tanzania zenye heshima inakwenda kukutana na wapinzani na jadi Simba Sports Club".
Mwisho akawataka mashabiki wa Yanga kuondoa mashaka kwani wataibuka na ushindi mkubwa. “Mashabiki wetu wa Yanga wasiwe na wasi waasi kambi iko vizuri tunaendelea vizuri, na tutaibuka na ushindi”.