Rais Samia amteua DPP Biswalo kuwa Jaji

Tuesday , 11th May , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani 7 pia amemuongezea muda Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani na ameteua Majaji wa Mahakama Kuu 21.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Mhe. Biswalo Mganga

Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Mhe. Biswalo Mganga, sasa atakuwa Jaji wa Mahakama Kuu.