Wakili wa kujitegemea nchini Tanzania Jebra Kambole
Kauli hiyo ameitoa kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kueleza kuwa hiyo ni miongoni mwa sera kandamizi kwa watoto wa kike kufikia malengo yao, na kudai kuwa wasichana hao wanapojifungua wanapaswa kupewe nafasi kwani wapo wengi waliowahi kukosea lakini walipopewa fursa walijirekebisha.
"Rais Samia pia aitolee mwongozo hii sera ya kwamba mtoto wa kike akipata ujauzito asirudi shule kwani ni kikwazo, sababu mtoto anapokuwa amepata ujauzito shuleni anakuwa ametendewa kosa la kijinai, lazima tufungue milango kwa wale wanaotaka kurudi shule watimize ndoto zao, watu wengi sana wanafanya makosa wanapewa fursa wanajirekebisha, ingekuwa watoto wa kiume ukitenda kosa unafukuzwa shule wangapi wangefukuzwa", amesema Wakili Kambole.

