Monday , 21st Jun , 2021

Atlanta Hawks imeshinda mchezo wa 7 (Game 7) kwenye mfululizo wa michezo ya nusu fainali Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, ukanda wa Mashariki dhidi ya Philadelphia 76ers, na kutinga hatua ya fainali ukanda wa mashariki.

Hawks imeshinda Game 7 dhidi ya Philadelphia

Hawks imeshinda michezo 4 kati ya michezo 7 baada ya alfajiri ya kuamkia leo kuinyuka 76ers kwa alama 103 kwa 96 na wametinga hatua ya fainali kwa mara ya pili kwenye fainali za kanda tangu timu hiyo ihamie Atlanta mwaka 1968.

Sasa watacheza dhdi Milwaukee Bucks kwenye mchezo wa fainali ukanda wa Mashariki, Bucks wametinga hatua hii baada ya kuitoa Brooklyn Nets katika mfululizo wa mchezo wa 7 Jumamosi iliyopita na mchezo wa kwanza wa fainali katika mfululizo wa michezo 7 ya fainali utachezwa siku ya Jumatano.