Wednesday , 30th Jun , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Juni 30, 2021, ameahirisha vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi Agosti 31 mwaka huu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Katiba hotuba yake hii leo Waziri Majaliwa, ameipongeza bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2021/2022 iliyopitishwa na Bunge hilo na kwamba ni miongoni mwa bajeti nzuri ambazo zimezingatiwa mahitaji na maslahi ya wananchi wa Tanzania.

Mbali na hayo Waziri Majaliwa pia, amewaomba Watanzania pamoja na wadau wa maendeleo kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ili iweze kutekeleza vipaumbele ilivyojiwekea katika kukuza uchumi wa nchi.