Thursday , 8th Jul , 2021

Kampuni ya Nice & Free Pads imechangia pedi kwa wanafunzi wa kike 85 watakaotumia kwa muda wa mwaka mmoja kupitia kampeni ya Namthamini ili waweze kupata hedhi za salama na kuendelea na masomo bila kuwa na hofu ya katika kipindi chote cha muhula wa masomo pindi wanapokuwa kwenye siku zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television na East Africa Radio Regina Mengi (Kushoto) akipokea mchango kwa ajili ya Kampeni ya #Namthamini kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Nice & Free Pads, Nice Kennedy (Kulia).

Akizungumza na EATV Mkurugenzi Mtendaji wa Nice & Free Pads, Nice Kennedy, amesema kama kampuni inayojishughulisha na usambazaji na uuzaji wa taulo za kike (Pedi), inatambua uhitaji mkubwa uliopo wa pedi kwa wanafunzi wa kike hususani katika maeneo ya vijijini hivyo kupitia kampeni hii wanafunzi wa kike wanakwenda kuwa na furaha ikiwa ni pamoja kuinua elimu yao.

Aidha, Mkurugenzi huyo amepongeza Kampeni ya Namthamini ya EAST AFRICA TELEVISION ikishirikiana na Flaviana Matata Foundation pamoja na uongozi mzima kwa kampeni hii, na kusema kwamba  inaenda kugusa na kuwainua watoto wa kike nchini ambao wanashindwa kuhudhiria masomo kutokana na kukosa taulo za kike.