Thursday , 12th Aug , 2021

Wachezaji wa klabu ya Chelsea ya England na timu ya taifa ya Italia, kiungo Jorginho na mlinzi wa kushoto, Emerson Palmieri wameweka rekodi ya kuwa wachezaji wa kwanza Duniani kubeba kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya, kombe la mataifa ya Ulaya na UefaSuper Cup ndani ya mwaka mmoja.

Emerson Palmieri (kushoto) akiwa na Jorginho wakishangilia baada ya Itali kuwa mabingwa wa Uefa Euros 2021 kwa kuichapa England kwenye penalti 4-2.

Rekodi hiyo ya kibabe kwa wawili hao imekamilika baada ya wawili hao kubeba ubingwa wa Uefa Super Cup kwa kuifunga timu ya nyambizi ya Hispania, Villareal kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 za mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye dimba la Windsor Park nchini Ireland.

Chelsea ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa winga wake, Hakim Ziyech dakika ya 27 ya mchezo kabla ya mshambuliaji wa Villareal, Gerard Moreno ajasawazisha dakika 73 na kulazimisha mchezo huo uende dakika dakika 30 za niongeza na hatimaye timu zikapigiana mikwaju ya penalti na Chelsea ikaibuka na ushindi wa penalti 6-5.

Bao la kusawazisha alilofunga Moreno limemfanya afikishe mabao 83 na kumpiku kinara wa upachikaji mabao kwenye historia ya klabu hiyo, muitaliano Guissepe Rossi na Moreno kuwa mfungaji mwenye mabao mwengi kwa sasa kwenye historia ya klabu hiyo.

Wachezaji wa Chelsea waliopata penalti ni Ceasr Azpilicueta, Marcus Alonso, Mason Mount, Jorginho, Christian Pulisic na Antonio Rudiger wakati Kai Haverts ndiye pekee aliyekosa penalti, tena penalti ya kwanza. Kwa upande wa Villareal, waliopata ni Gerard Moreno, Pervis Estupianan, Mpoi Gomez, Juan Foyth, Daniel Raba ilhali Aissa mandi alikosa penalti ya pili na nahodha, Raul Albiol alikosa penalti ya mwisho.

Kwa upande wa rekodi nyingine, Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amekuwa kocha wakwanza kwenye  timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa na Uefa Super Cup. 

Mafanikio ya Emerson na Jorginho yamezidi kuwafanya waendelee kuwa na hamu ya kuanza msimu ili kufukuzia medali na makombe mengine baada ya kuweka rekodi hiyo ya kibabe kwasasa.