Thursday , 12th Aug , 2021

Bingwa wa zamani wa uzito wa juu, David Haye ametangaza kurejea ulingoni ikiwa ni miaka mitatu tangu astaafu mchezo huo na atapambana na Joe Fournier Septemba 11 mwaka huu huko Staples Center katika Jiji la Los Angeles nchini Marekani.

Bingwa wa zamani wa uzito wa juu,David Haye enzi zake akiwa ulingoni.

Haye ambaye hajapanda ulingoni tangu apoteze pigano kwa mara ya pili dhidi ya Tony Bellew mwaka 2018,atapigana na Joe katika pambano la raundi 8.

Tangu astaafu, bondia huyo amekuwa akimsimamia mpinzani wake wa zamani katika masumbwi ,Derek Chisora.

Akizungumzia juu ya pigano hilo,Haye amesema alitwaa ubingwa wa dunia miaka 10 iliyopita na anaamini katika umri wake wa miaka 40 anauwezo wa kufanya makubwa katika pambano hilo.