
Picha ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa
Waziri Bashungwa amesema kwa nia njema ya kukuza sanaa ni lazima wasimamie mila, desturi na maadili ya nchi na hakuna Taifa ambalo halina utambulisho wa mila na desturi.
Aidha amesema kuhusu suala la maadili na kufungiwa kwa wasanii hawataweza kukubali kwa sababu ya kutaka kukuza sanaa na kutengeneza ajira, na wataendelea kusimamia sheria kwa wasiofuata taratibu.