
Kushoto Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa, Kulia ni nMbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima
Kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge Leo jijini Dodoma imeeleza kuwa Mhe. Gwajima anatakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo siku ya jumatatu tarehe 23, Agosti 2021 saa saba mchana huku Mhe. Silaa akitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo tarehe 24/08/2021 saa saba kamili mchana katika ofisi za Bunge.
Kwa mujibu wa kanuni 4(1) (a) na (b) ya nyongeza ya nane ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Juni 2020 ambayo inaipa mamlaka Kamati hiyo kuchunguza mambo yanayohusu maadili yanayopelekwa na spika, hivyo basi wabunge hao wanatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo.
Aidha endapo waheshimiwa hao hawatafika mbele ya kamati kwa siku na muda uliotajwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.