Monday , 23rd Aug , 2021

Msanii wa singeli Manfongo anasema mtu akimiliki gari inaongeza chuki kwa watu wengine kwa sababu huonekana kama anaringa hata akisalimia watu anaweza asiitikiwe salamu yake.

Manfongo ameeleza kuwa mtu asiyemiliki gari anakuwa na makasiriko zaidi kuliko yule ambaye ana miliki gari yake.

"Mtu asiyemiliki gari anakuwa na hasira sana kuliko anayemiliki gari kwa sababu gari linajenga chuki, unaweza ukapaki gari lako kusalimia watu wasikuitikie na utaonekana unaringa kisa umeenda na gari" amesema Manfongo 

Manfongo ameongeza kusema yeye ndio msanii wa kwanza wa singeli kumiliki gari aina ya Altezza na sasa anakamilisha mjengo wake maeneo ya Kimara Saranga.

Zaidi tazama hapa kwenye video akizungumzia suala hilo.