Tuesday , 9th Nov , 2021

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema Bunge limechoka kusikia mradi wa Liganga na Mchuchuma bila mafanikio na kuipa serikali miezi 3 kabla ya Bunge la 2022 na kama ikipita hawajasema chochote cha maana kwa mradi huo basi Bunge watachukua jukumu kwa kuunda tume teule ili walivae wenyewe.

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Kauli hiyo ameitoa Bungeni na kusema ni miaka mingi Bunge limeomba mradi huo kujua unavyotekelezwa lakini hakuna majibu ya kueleweka ili wananchi  waelewe kuhusu mradi huo ambao nao bado hawajaujua ulivyo.