
(Mlinzi wa kati wa Yanga SC, Dickson Job (kulia) alipokuwa anasaini mkataba wa kujiunga na Yanga Januari 2021.)
Job anayecheza sambamba na nahodha wake, Bakari Mwamnyeto kwenye pacha ya walinzi wa kati amesema, viungo wao wakabaji walio bora, Yannick Bangala na Khalid Aucho wamewafanya wasiwe na kazi kubwa ya kulinda lango lao na kumsaidia kipa wao Djigui Diarra asifikike kirrahisi.
Beki huyo kitasa amesema: “Tunacheza na walimu kiwanjani. Ukiachana na kocha Nabi, tumeongezewa nguvu kubwa ambayo imekuwa na msaada kwetu. Hatufanyi makosa ya kizembe ndiyo maana unaona tulivyo imara katika Ulinzi”.
Yanga kwa sasa inaongoza Ligi kuu ya NBC Tanzania kwa kuwa na alama 15, ushindi wa asilimia mia katika michezo yake mitano wakiwa vinara wa ufungaji wakiwa na mabao 9 na kuruhusu kufungwa bao moja pekee.
Na kwenye michezo hiyo, Dickson Job amecheza michezo yote, mara moja akicheza na Yannick Bangala na mara nne na Bakari Mwamnyeto kwenye eneo la ulinzi.