
Dean Smith, Kocha mpya wa Norwich City.
Kocha huyo mwenye umri wa 50, anarithi mikoba ya Daniel Farke, ambaye alitimuliwa na Canaries wakiwa mkiani mwa EPL na sasa Craig Shakespeare, ambaye alifanya kazi na Smith Villa Park, ataungana naye kama msaidizi wake katika vya viunga Carrow Road.
Katika miaka mitatu akiwa Villa, Smith aliwaongoza kupanda daraja kutoka Championship hadi ligi kuu ya England na kufika fainali ya Kombe la Carabao 2020.
Mchezo wa kwanza wa Smith utakuwa nyumbani dhidi ya Southampton tarehe 20 Novemba ambapo ataweka historia ya kuwa Kocha wa kwanza kuongoza timu mbili tofauti dhidi ya mpinzani mmoja kwenye mfululizo wa mechi za EPL , baada ya kutimuliwa na Villa kufuatia kufungwa na Saints.
Kwa upande wa Norwich ilimfukuza Farke mnamo 6 Novemba baada ya ushindi dhidi ya Brentford, ambao ulikuwa ushindi wa kwanza wa ligi msimu huu.
Ikumbukwe kuwa Meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard pia alifanya mazungumzo na Canaries, lakini akajiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.