
(Gwiji wa Brazil, Pele)
Pele amerudi kwenye Hospitali hiyo ambayo alikuwa anatibiwa tokea Agosti 31, 2021 hadi kufanyika upasuaji mwingine mwezi Septemba mwaka huu wa kumtoa uvimbe kwenye utumbo wake mkubwa.
Baada ya matibabu hayo, Hospitali hiyo imeeleza kuwa haliya Gwiji huyo inaendelea vizuri kwasasana siku chache zijazo ataruhusiwa kurudi nyumbani
Pele amekuwa na kipindi kigumu kwa kuandamwa na maradhi kwani mwaka 2015 alifanyiwa upasuaji wa tezi dume baada ya kulazwa kwa miezi sita na mwaka 2019 kufanyiwa upasuaji wa mfumo wa mkojo.
Pele ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Brazil kwa kufunga magoli 77 kwenye michezo 92na miongoni mwa wachezaji wachache waliofunga kwenye michuano mine tofauti ya kombe la dunia.