kocha Jose Mourinho
Hiki kilikuwa ni kipigo cha kwanza kwa Jose Mourinho kwenye michezo 5 ya mwisho kwenye mashindano yote walioshuka dimbani. Mchezo huu ulichezwa katika dimba la San Siro na wenyeji AC Milan walikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 8 kupitia kwa Olivier Giroud aliyefunga kwa mkwaju wa penati, Milani wakafunga bao la pili dakika ya 17 kupitia kwa Junior Messias, dakika ya 40 Tammy Abraham akaifungia Roma bao kabla ya Rafael Leao kufunga bao la 3 kwa AC Milani na kuihakikishia ushindi dakika ya 81.
AC Milan imefikisha alama 45 katika michezo 20 wakiwa nafasi ya pili, ikiwa ni tofauti ya alama 1 dhidi ya vinara Inter Milan wenye alama 46 wakiwa wamecheza michezo 19. Kwa kipigo hiki Roma wamesalia nafasi ya 7 wakiwa na alama zao 32 ikiwa ni tofauti ya alama 6 dhidi ya Atalanta wanaoshika nafasi ya 4 ambayo inatoa tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa lakini pia ni tofauti ya alama 14 na vinara Inter Milan.
Kwa ujumla Jose Mourinho amekiongoza kikosi cha Roma kwenye michezo 28 kwenye mashindano yote, na kipigo dhidi ya AC Milan kilikuwa ni cha 8 kwenye Serie A na cha 9 kwenye michuano yote huku akiwa ameshinda michezo 16 na sare michezo 3 wastani wake wa ushindi akiwa na kikosi hi ni asilimia 57.14.
Matokeo ya michezo mingine ya Serie A’iliyochezwa jana.
Juventus 1 – 1 Napoli
Sampdoria 1 – 2 Cagliari
Lazio 3 – 3 Empoli
Spezia 1 – 2 Verona
Sassuolo 1 – 1 Genoa
