Friday , 7th Jan , 2022

Kocha wa Simba SC Pablo Franco Martin amesema atafanya mabadiliko kwenye kikosi chake kuelekea mchezo wa usiku wa leo dhidi ya Mlandege kwenye michuano ya Mapinduzi CUP, na ameweka wazi kuwa atawapa nafasi ya kucheza wachezaji walio kwenye kikosi hicho kwa ajili ya majaribio.

Wachezaji wa Simba wakishangilia goli

Simba itashuka Dimbani leo Usiku Saa2:15 kwenye mchezo wa kundi B, na kuelekea mchezo huo kocha wa kikosi hicho Pablo Franko amesema

“Hatukupata muda wa kujiandaa lakini tunapaswa kushinda kila mchezo. Tutafanya mabadiliko kidogo ya kikosi kwa ajili ya kuwalinda wachezaji. Tumeongeza wachezaji wengine kwa ajili ya majaribio ambao tutawatumia katika mashindano haya na wakituvutia tutawapendekeza kwa uongozi wasajiliwe.” amesema Pablo.

Tayari kikosi cha Simba kimefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya mapinduzi. Lakini mchezo wa mapema leo unachezwa Saa 10:15 Jioni Yanga SC watacheza dhidi ya KMKM, michezo yote hii inachezwa katika dimba la Amaani