Wednesday , 2nd Mar , 2022

Nyota wa tennis Mserbia Novak Djokovic ameachana na mkufunzi wake raia wa Slovakia Marian Vajda baada ya kudumu kwa kipindi cha miaka 15 huku mara ya kwanza kwa wawili hao kufanya kazi ilikuwa mnamo mwaka 2006.

Nyota Novak Djokovic akiwa na kocha wake wa zamani Marian Vajda

Djokovic mwenye umri wa miaka 34 walipanga kufikia tamati ya kimkataba na kocha Vajda mwishoni mwa msimu wa mwaka 2021 huku mkufunzi huyo akimpa mataji matatu ya Grand Slam.

"Marian amekuwa upande wangu kwenye nyakati zote nzuri na za kukumbukwa kwa kipindi chote cha maisha  yangu kwenye tennis ,kwa pamoja tumeshinda vitu vingi na namshukuru kuwa rafiki wa kweli kwa kipindi cha miaka 15”amesema Djokovic.

Hii itakuwa ni mara ya pili kutengana kwa wawili hao  kama ilivyokuwa mwaka 2017 kisha kurejeana tena mwaka 2018 huku mwaka 2022 umekuwa mgumu kwa Novak Djokovic ambaye alizuiwa kushiriki kwenye michuano ya Australian Open 2022 na kushuka nafasi ya kwanza jumatatu hii  iliyokwenda kwa Mrusi Daniil Medvedev.